AWAMU YA NNE YA MIKUTANO YA TUME YA KATIBA KUKUSANYA MAONI YAANZA LEO KATIKA MIKOA SITA.

Na.Mo Blog Team

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Jaji Joseph Warioba akitoa maelezo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tume hiyo kuendelea na awamu ya nne ya mikutano yake ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Arusha, Simiyu, Geita, Mara na Mjini Magharibi itakayofanyika hadi Desemba 19 mwaka huu.

Amesema taratibu zote za kuanza kazi ya kukusanya maoni katika mikoa iliyotajwa zimekamilika zikiwemo kuandaa ratiba na kuisambaza katika ofisi za mikoa, wilaya na halmashauri za manispaa na wilaya husika.

Aidha Jaji Warioba amesema Tume hiyo inatarajia kukutana na wadau kutoka taasisi mbalimbali ili kupokea maoni ya kuhusu katiba mpya, na tayari Tume imesha andaa ratiba ya kukutana na Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Asasi za Kidini, Vyama vya Kitaaluma, Vyama vya Wakulima, Wafanyakazi na Wafanyabiashara pamoja na wadau wengine wakiwemo watu mbalimbali wenye uzoefu katika masuala mbalimbali.

Pia ametumia fursa hiyo kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuwa anaamini vina mchango mkubwa sana katika kufanikisha mchakato mzima wa kuandaa katiba mpya.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional