Maafisa ugani mkoa wa Singida wapatiwa pikipiki mpya 11 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 90 kwa ajili ya kuwarahishia usafiri.

Katibu tawala msaidizi mkoa wa Singida,Aziza Mumba akitoa taarifa yake ya makabidhiano ya pikipiki 11 za maafisa ugani kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi,funguo za pikipiki zilizokabidhiwa maafisa ugavi.

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,akijaribu kuendesha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maafisa ugani mkoani Singida.

Baadhi ya pikipiki zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 90 zilizokabidhiwa kwa maafisa ugani.Picha na Nathaniel Limu.

Na Nathaniel Limu.

Serikali kwa ushirikiano na shirika la maendeleo la Japan (JAICA)imeupatia mkoa wa Singida jumla ya pikipiki 11 mpya, zenye thamani ya zaidi ya shilingi 90 milioni kwa ajili ya kuwarahishia usafiri maafisa ugani.

Hayo yamesemwa na katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani Singida Aziza Mumba, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi pikipiki mpya kwa halmashauri za wilaya na manispaa.

Amesema pikipiki hizo ni kwa ajili ya kuwawezesha maafisa ugani kuratibu utekelezaji wa mipango  ya maendeleo ya sekta ya kilimo (DADPs).

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, amewataka wataalamu watakaokabidhiwa pikipiki hizo, watambue kwamba wanalo deni kubwa la kuhakikisha kuwa malengo ya kupatiwa pikipiki hizo yanafikiwa.

Akifafanua, amesema lengo ni kuwatumikia ipasavyo wananchi na kuwafanya wajiletee maendeleo yao kupitia sekta ya kilimo.

Kwa mujibu wa Aziza, mkoa wa Singida kwa sasa una pikipiki 88 za maafisa ugani sawa na aslimia 49 ya lengo la kuwa na pikipiki 181.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional