Dkt. Bilal azindua Rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Karimjee Dar leo.

9

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, maalum kwa uzinduzi huo.

01

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba. (Picha  zote na Ofisi ya Makamu wa Rais).

03

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

04

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.

06

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.

07

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.

08

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, wakiperuzi kitabu cha Katiba mpya, baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo kwenye Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.

1

Mwimbaji wa bendi ya Mjomba, Ismail (katikati) akiimba na kucheza pamoja na wanenguaji wake, kutoa burudani wakati wa shambra shambra za uzinduzi huo.

4

 Baadhi ya wazee waasisi waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo leo.

8

Sehemu ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, waliohudhuria hafla hiyo, wakiwajibika.

 

09

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, baada ya uzinduzi huo.

10

 Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.

11

Makamu wa Rais, Dkt. Bilal (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Salim Ahmed Salim, wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo baada ya uzinduzi.

 
 
 

About the author

More posts by

 

8 Comments

 • Kazi muliyotumwa na Taifa mmeifanya kwa uadilifu mkubwa. HONGERA SANA!!. Kamilisheni lililobakia itoke Katiba nzuri na vizazi vijavyo vifurahie.

   
 • martin elia

  kweli hapo ndio tunapo pataka tuhakikishe hakuna udini hata kidogo na kila mtu aabudu dini yake bila kuathiri dini nyingine na kila mtu ajue kuwa nchi hii ni ya wote wala haitakuwa ya dini fulani hata kama kuna mtu anafikiria hivyo
  vile vile viongozi na wananchi wote ambao wanachochea udini na wakagundulika wanyongwe ili watuachie jamuhuri yetu salama.
  mungu bariki tanzania mungu tubariki watu wa nchi hiii ameeeee

   
 • sinior citizen

  Babaraza ya katiba, na Bunge la katiba watakuwa na kazi ya ziada ya kuongezea mapungufu katika kazi nzima iliyofanywa na Tume ya Katiba bila kuathiri mchoro mzima mliouweka.

   
 • sinior citizen

  Natumaini Baraza la Katiba na Bunge la Katiba watokuwa na kazi ya ziada ya kuongezea pale penye mapungufu ya msingi, bila kuathiri msingi wa mchoro mzima wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyouweka.

   
 • Ali Mohammed

  Mimi naona kwamba hao wanaosema eti chama chetu sera yake serikali mbili hayo ni maoni ya chama sio watanzania sasa watanzania waliowengi wanataka kila upande uwe na serikali yake hivyo bora tukubalianae na rasimu ilivyo anza iwe serkali tatu kwa kuanzia

   
 • Mimi naona hiyo sera ya serikali mbili nikama njia ya kuaharibu mchakato kwa sababu sasaivi watanzania wanatakiwa wachanigie rasimu na sio mambo yaliyokuwa nje ya rasimu

   
 • prosper juma

  ukweli katiba ni nzuri, lakini bado tunahitaji ufafanuzi kuhusu muundo wa serikali3.

   
 • Tchamassoum Veronique

  Big up. Kwa kweli katiba ni nzuri. Hongera kwa tume. Malalamiko ni kama kujiangalia kwenye kioo, unaona kumbe una chunusi. Basi, zishughulikieni. Itakua nzuri. Tunawaombeeni dua wana kamati ya tume ya katiba.

   
 

 

Add a comment

required

required

optional