Halmashauri ya manispaa ya Singida inatarajia kuvuna ziada ya chakula zaidi ya tani elfu 15 katika msimu huu wa kilimo.

DSC02140-2140

Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joseph Mchina,akitoa taarifa yake ya utekelezaji ya mwaka 2012/2013 mbele ya kikao maalum cha baraza la madiwani juzi.Wa pili kulia ni Mustahiki meya wa manispaa ya Singida na Sheikh wa mkoa wa Singida,Salum Mahami.Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida,Hamisi Nguli na anayefuatia ni makamu meya manispaa ya Singida,Hassan Shabani Mkata.

Halmashauri ya manispaa ya Singida inatarajia kuvuna ziada ya mavuno ya chakula tani 15,833 katika msimu huu wa kilimo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Joseph Mchina wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 mbele yab kikao maalum cha baraza la madiwani .

 Amesema kwa msimu huu wa kilimo, walitarajia kulima hehta 14,475 za mazao ya chalua na wanatarajia kuvuna tani 33,333 wakati mahitaji halisi ni tani 17,500.

 Aidha Mchina amesema kwa upande wa mazao ya biashara, wanatarajia kuvuna tani 10,700.

Katika hatua nyingine, kikao hicho kimemrejesha madarakani makamu meya wa manispaa hiyo Hassan Shabani Mkata, kwa kumpigia kura zote 18 za ndio.

Mkata hakuwa na mpinzani.

 Pia kikao hicho kimechagua kamati mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.

 Kamati ya fedha na utawala itaongozwa na Mstahiki Meya na Sheikh wa mkoa wa Singida,Salum

 Kamati ya uchumi,afya na elimu itakuwa chini ya Gwae Mbua na wajumbe wake ni Hamisi Nkulungu,Pantaleo Sorogai,Mwajuma Shaha,Shabani Kiranga na Hamisi Kisuke.

 Kamati ya kudhibiti UKIMWI,itaongozwa na makamu meya Hassan Shaban Mkata na wajumbe wa kamati hiyo ni,Magreth Malecela,Baltazari Kimario,Hadija Simba na wajumbe nane kutoka makundi mbali mbali maalum.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional