Mohammed Dewji ‘MO’ alizaliwa tarehe 8/05/1975 , mjini Singida kata ya Ipembe. Ni kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mo alizaliwa salama, kwani mama yake mzazi alijifungua akiwa nyumbani lakini alisaidiwa na nesi na daktari. Ni mtoto wa pili wa Mzee Gulam Dewji katika watoto sita wa familia hiyo. Ana dada mmoja Sabera na wadogo zake Ali, Hassan, Hussein na Fatema.
Baada ya kufikisha umri wa miaka mitano, alihama na kwenda mkoa wa Arusha kwa ajili ya elimu ya shule ya msingi. Aliishi Arusha na kusoma katika Shule ya msingi ya Arusha hadi mwaka 1986 alipohitimu elimu ya msingi.
Mwaka 1987 alihamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya sekondari na alijiunga na shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST), hapo Mo alimaliza elimu yake ya Sekondari mwaka 1992. Na huu ndio ukawa mwisho wake wa kusoma nchini Tanzania .
Mwaka 1992 alienda kuongeza elimu mara hii akisafiri kwenda nje ya nchi kutafuta elimu na kufanikiwa kuingia katika Shule ya SaddleBrooke High School ya Marekani. Akiwa hapo ndipo Mo alipoanza kuonyesha dalili za kwanza za kuwa na sifa za uongozi pale aliposhika nafasi ya kuwa Rais wa wanafunzi wa shule ya SaddleBrooke. Kushika nafasi kama hiyo katika nchi ngeni lilikuwa ni jambo la kujivunia na heshima kubwa kwa familia na pia Watanzania kwa ujumla. Pamoja na kuwa na nafasi ya uongozi akiwa shuleni Marekani, Mo alipigiwa kura hapo shuleni ya kuwa kati ya wanafunzi waliofanya vizuri au tunaweza tukasema wenye vipaji( Most Accomplished student) na upande wa wanawake aliyepigiwa kura hapo mwaka huu alikuwa ni mchezaji maarufu wa tenisi duniani wakati ule Jeniffer Capriati.
Alipomaliza elimu yake hapo Saddle Brooke , Mo alipata nafasi ya kujiunga na moja kati ya vyuo vikuu bora duniani, GeorgeTown University iliyokuwa jijini Washington D.C, Marekani. Alisomea mambo ya biashara ya kimataifa na fedha, huku akichukua Theolojia kama somo la ziada.
Katika kipindi hicho cha masomo katika chuo cha GeorgeTown ndipo Mo alipoanza kubadilika kimaisha na kubadili mtazamo mzima wa kuangalia mambo ambayo binadamu anayafanya kila siku. Chuo hicho kinasifika kuwa na elimu bora na kimetoa viongozi na watu ambao wamefanikiwa sana katika maisha mfano Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Mfalme Abdullah wa Jordan, Rais Gloria Arroyo wa ufilipino na hata wachezaji wa mpira wa kikapu maarufu nchini Marekani kama Allen Iverson na Patrick Ewing.
Alipohitimu masomo mwaka 1998 alirudi nyumbani Tanzania na moja kwa moja akaingia kwenye biashara za baba yake Mzee Gulam na akaanza na nafasi ya Mdhibiti mkuu wa Fedha katika kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL).
Mbali na kuingia kwenye biashara, Mo alijiingiza kwenye michezo na kuanza kuifadhili Simba Sports Club ya Dar es Salaam. Huu ukawa mwanzo wa Watanzania kumuona Mo akiingia kwenye ulimwengu wa michezo wa Tanzania na hasa soka.
Ilipofika mwaka 2000, uchaguzi wa pili wa mfumo wa vyama vingi nchini uliwadia. Na Mo akajiingiza kwenye kinyanganyiro hicho akiwania kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Singida mjini. Katika kura za maoni Mo alimshinda Waziri wa Maji wa wakati huo Musa Nkhangaa kwa kura nyingi lakini kamati kuu ya CCM hawakumpitisha kugombea ubunge.
Kuna usemi mvumilivu hula mbivu, hivyo Mo akakubali na kuheshimu maamuzi ya chama na kumpigia kampeni mgombea wa chama na kuhakikisha wanashinda Uchaguzi wa 2000.
Pamoja na kushindwa kupata nafasi ya kugombea ubunge, Mo aliwasaidia wananchi wa Singida kwa hali na mali , huku pia akizidi kutoa mikataba minono ya udhamini kwa Simba iliyokuwa inazidi Milioni mia moja kwa mwaka.
Mwaka 2001 Mo aliamua kuachana na ukapera na kuamua kumuoa Saira, ambaye walijuana tokea enzi za shule. Kila kitu kinapangwa na Mungu kwani Mo alienda kusoma Marekani na kupoteza mawasiliano na Saira, lakini aliporudi kutoka Marekani ndipo wanandoa hao walianza kujuana zaidi na hatimaye kuamua kufunga ndoa ambapo wamejaliwa kuwa na watoto wawili, mmoja wa kike aitwaye Naila mwenye umri wa miaka sita na wa kiume anaitwa Abbas mwenye umri wa miaka mitatu.
Miaka miwili baada ya ndoa Mo alipanda cheo katika kampuni ya familia na kukabidhiwa rasmi kampuni nzima kama Mkurugenzi mkuu wa Mohammed Enterprises Limited (METL). Chini ya uongozi wake kampuni imepanda ngazi nyingi za mafanikio na kukua mara nane ya kiwango alichokikuta kuanzia pale alipoanza kufanya kazi, amewekeza kwenye sekta tofauti kama Kilimo, Fedha, Uzalishaji na Usambazaji wa bidhaa.
Takwimu zinaonyesha kampuni za Mo zinachangia pato la ndani la taifa kwa asilimia mbili na zinaajiri zaidi ya watu 20,000.
Mwaka 2005 ulikuwa mwaka wa uchaguzi na MO akachukua fomu tena za kuwania ubunge wa jimbo la Singida mjini. Kwa mara nyingine aliibuka kidedea katika kura za maoni akipitishwa na kamati kuu ya CCM kuwa mgombea na baada ya hapo akawabwaga wapinzani wake katika uchaguzi kwa kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia tisini ya kura zote zilizopigwa.
Tarehe 29 /12/2005 Mohammed Dewji ‘Mo’ aliapishwa kuwa Mbunge wa Singida mjini, na kuwa mwakilishi rasmi wa kero za wananchi wa Singida mjini bungeni.
Michezo na Mo hawakai mbali mbali. Rais Kikwete alikuja na ari mpya na kuwafanya Watanzania kupenda michezo na hasa timu yao ya taifa ya soka, Taifa Stars. Ili kufanikisha na kuleta maendeleo ya Stars kamati maalumu ya ushindi iliundwa huku Mo akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wake. Katika kipindi chake Taifa Stars wamebadilika kutoka kuwa kichwa cha mwendawazimu na kuwa timu inayoheshimika barani Afrika ikitoa sare na vigogo wa soka kama Cameroon na Senegal .
Pia chini ya uenyekiti wake Taifa Stars imepata kushiriki michuano mikubwa barani Afrika ya CHAN yaliyofanyika nchini Ivory Coast .
Mwaka 2007 kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama (CCM) na Mo alijitosa na kuwania kugombea nafasi ya mjumbe wa Halmashauri ya taifa (NEC) na akafanikiwa kushinda kwa kupata kura za kutosha na kuweza kufanikisha azma yake hiyo.
Hii ni historia fupi ya Mhe. Mohammed Dewji ( Mbunge, Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC) na mkurugenzi wa makampuni ya Mohammed Enterprises) ambaye anaendelea kusaidia jimbo na taifa lake kwa hali na mali pale anapokuwa na uwezo na nafasi ya kufanya hivyo.










at 12:18 am
TUNAITAJI VIONGOZI WAZURI KAMA MO, NA KAMA CCM INATAKA KUBAKI MADARAKANI BASI HUYU ANAFAA KUWA KIONGOZI NA RAIS WA TANZANIA
at 7:21 am
tunajivunia kuwa na watu kama hawa ambao ni watanzania wachache wenye uwezo wa kimali na hawajikwezi na wako tiyari kuawana kile walicho nacho kwa watanzania wenzao Mola akulipe na akuongezee ulicho nacho AMIN……….
at 9:57 pm
Kaka unastahili na ninakuombea uendelee na moyo wako wa kusaidia jamii nzima hasa sisi masikini.
at 9:38 am
Nakupongeza kwa hayo yote, pamoja na hayo napenda kujua kero zetu za maji, ajira na kiuchumi kwa sisi wanasingida huzioni au?
Je unapenda wamama wanavyoteseka kusaka maji badala ya kufanya shughuli zingine za kimaendeleo?
Tafadhali tunaomba weka japo kiwanda kimoja hii itatoa mchango mkubwa sana kwa kuwapa ajira wanasingida japo za kiwandani.
Usijikite dsm peke yake, tunaomba ufikishe kero zetu bungeni, muda mrefu sana tangu uonge mara ya mwisho bungeni, kama una mapenzi ya kweli na singida utayafanyia kazi hayo nayokuambia.
at 3:10 pm
Mimi naishi hapa mjini,aliyoyafanya mhe.Mbunge yamewagusa wananchi wa chini sana,tuliyesimamia uchaguzi tunafahamu,nafikiri maelezo ninayo ya kweli na yenye ushahidi.
at 9:47 am
kwakel dewj nakukubal asilimia 100,na unafaa kuwa kiongoz mkubwa sana ktk taifa hili na unajali sana wanainch wako lakin mh,dewji naomba uangalie sana swala zima lakuwasaidia watoto yatima na wanoishi katika mazingira magumu hasa katika suala zima la kielimu,singida iko nyuma sana kielim ukikompea na mikoa mingine pia ni mkoa maskin sana hili tatizo linachangiwa sana na ukosefu wa elimu na ajira kwa vijana naomba hili suala uliangalie kwa pande zote negative effect na possitive side,mm napata uchungu sana kuona watoto yatima na wanaoish katika mazingira magumu wanateseka sana especially watoto wa kike,wasichana wengi hasa wanaotoka mkoa sgd waishia kuwa mabarmedi na wasichana wenye umri chin ya miaka kumi na tano wanaishia kuwa mahouse girls kuhusu hili suala utatusaidiaje?endapo vijana wengi watapata elimu inawezekana kabisa sgd kupata maendeleo kwa kasi kwakuwa kila mmja atakuwa anajua nn maana ya maendeleo sio sawa na wale wasioenda shule ninameng sana lakin kwa leo naishia hapa
at 7:14 am
good mr.DEWJI
at 9:42 am
Mo hongera sana, ila please najua una uwezo, majuzi nlikuwa singida nimewaona akina mama watu wazima na wananchi wote wa singida wanahangaika sana kupata maji hasa muda kama huu ambapo umeme ni wa tabu na mitambo ya idara ya maji haifanyi kazi. Na hata umeme ukiwepo vizima vingi vimekauka, kwa kweli ukiweza (na nina uhakika unaweza) kuwasaidia ndugu zako, vijana wenzako na wazazi wako hapa singida kupata maji safi na salama nina uhakika utapata baraka nyingi sana toka kwa mola wako. Wote tunafahamu pepo ya mungu ipo miguuni mwa wazazi wetu, ebu month tusaidie tulifanikishe hili na utabarikiwa, ameen.
at 9:50 am
Kwa ushauri, sio uchimbe visima tu then uviache hivyo, bora kuviunganisha kwenye mabomba ya idara ya maji ili maji hayo yawafikie wananchi wako wa singida
at 10:32 am
Mh. Mo. Hakika, katika watu walioweka historia kwenye jamii yetu, wewe ni mmojawapo. Binafsi, nathamini sana juhudi zako katika kuleta maendeleo. Lakini, waswahili husema, “NATENGEZA KWA WENZANGU, KWANGU KUNAPOROMOKA”. Simaanishi kuwa hujafanya chochote Singida, la! Ila, kama ungeamua kwa dhati kufanya kweli, pale Singida sasa hivi ungekuta pamebadilika kwa kasi. Ushauri wangu, kama utaona sawa ni huu:-
1. Anzisha chuo cha maendeleo ya uchumi(unaweza kuweka kitaalamu zaidi)Elimu ya jamii ikikaziwa sana.
2. Elimu ya Vijana kujitambua, kwamba wao ni nani, wanaelekea wapi, na wanatakiwa kufanya nini.
3. Viwanda vya uzalishaji kama vya Dar es Salaam (Hata kama havitakuwa vikubwa kama vya Dar), vinaweza kuajiri vijana wengi, ambao wanaweza kufundishwa direct kazini. Isipokuwa kwa nafasi nyeti ndipo waajiriwe wataalamu maalumu.
4. Uanzishaji wa Hoteli kubwa za kitalii (kwa kuwa tunafanya mipango ya kukuza Utalii Singida). Hata wakati watalii hawajawa wengi, kumbuka barabara za lami toka Arusha kuja Singida mpaka Mwanza zinarahisisha usafiri.
5. Upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Singida, kuweza kutua ndege za kibiashara.
6. Elimu kwa vijana juu ya rasilimali za Singida, waweze kuongoza watalii.
Utaona hapa kuna maandalizi ya muda mfupi na ya muda mrefu. Hata kama kizazi chetu kitapita, kijacho kitaendeleza.
Nakuombea maisha marefu na uendelee na moyo huo huo.
at 10:09 am
thats gud and keep it up kwani Tanzania ya leo itajengwa na sie vijana kwa kuonesha nia ya kuisaidia nchi yetu,
tunahitaji viongozi bora na wenye nia thabiti
at 10:16 am
Vyote ulivyofanya ni nzuri.Watu wa sgd hawahitaji kupewa pesa hata kwa umasikini walionao ila wanahitaji kuwezeshwa kielimu ili waweze kuitumia kujikwamua na maisha. Nasema hivi kwa vile wamejenga shule nyingi za kata kwa umasikini wao huo tofauti na mikoa mingine lakini shule hizo hazina walimu na vitabu vya kufundishia,ingekuwa ni vyema mkakaa na wenzio mjue ni namna gani mtaweza kutatua hili hapo tutakuwa na singida yenye neema tofauti na hivi sasa.
at 8:31 am
We need people who can encourage our citizens to move forward and make a difference in our Country.Big Up Brother.
at 8:49 pm
Thumbs up! great stuff you doing out there.Am impressed.
at 10:30 am
Ongera mheshimiwa, na sisi wana msimbazi tunakuhitaji uje uendelee na ufadhili.
at 4:25 pm
HONGERA KAKA KWA JUHUDI NA MAFANIKIO ULIYOYAPATA,LAKINI NINAUSHAURI MDOGO TU,KAKA SIASA ZA AFRIKA ZINAMATATIZO,NI VIZURI UNATUWAKILISHA MANYONGE ILA IFIKE WAKATI JIUPUSHE NA SIASA UFANYE MAMBO MENGINE,ILI KUEPUKANA NA MATATIZO YA SIASA CHAFU AMBAZO ZINATUNYEMELEA TANZANIA,NI HAYO TU NAKUTAKIA MAISHA MEMA USIMSAHAU MUNGU WAKUMBUKE MASIKINI.
at 8:31 pm
HONGERA, UNA ELIMU NZURI, UNA UPEO NA NAFAHAMU UWEZO WAKO NI MKUBWA KWA KILA KITU MSHUKURU SANA MUNGU KWA HILO
at 9:44 am
MO NAKUIOMBA KITU KIMOJA TBL WAMENIUDHI SANA KUMBE WANAGADHILI MICHEZO KWAAJILI YA BIASHARA ZAO TUU KITENDO CHA KUZIFADHILI SIMBA NA YANGA MAMILIONI YA PESA NA KUZARAU TIMU NYINGINE ZA LIGI KUU NAONA SI CHA KIUNGWANA ACTUALY SIO KENDELEZA SOKA BALI NI KUDIDIMIZA SOKA NCHINI NAOMBA TUMIA UWEZO WAKO KUSHAURI BODI YA TBL IZIJALI NA TIMU NYINGINE NA HASWA ZA NIKOANI KWAKUNWA WANYAWAJI WA BIA HAPO DAR TUU KWANINI WAPENDELEE UPANDE MMOJA TUU. YOUR TAGGED CHAT MAT NAJUA MANAZI WATACHONGA SANA KWA HILI LAKINI ACHANA NAO
at 12:54 pm
May GOD be wih u always brother, Ki ukweli ur presence is seen in all ways. Keep it up we shall follow ur steps brother.
at 2:53 pm
Bro… nimekusoma vizuri sana endelea kumwomba ALLAH akupe moyo wa kushuka zaidi ili upate kuwa hudumia wananchi zaidi ya hapo,Mchango wako binafsi nimeuona kwa serikali ya Tz hasa kwenye michezo BABU.
Naweza kusema kati ya watu ambao wamefanya Watanzania angalau waonekane katika Tansania ya michezo wewe nimmoja wapo,kama ni kiungo wa mpira basi naweza kusema wewe ulikuwa namba six,lakini Babu pamoja na hayo saizi sikusikii kwenye hiyo Tansia ya michezo au ndo kusema tenda wema uende zako?
By the way Babu mimi nakupa big up… endelea na songa mbele kabisa.
Nashukuru sana ila Babu singida bado wana shida na maji,sijuwi unawafikiriaje? kisha waambie wapande miti mingi maake nahisi ndani ya miaka thelathini ijayo panaweza kuwa jangwa na pakiwa jangwa,..Babu utawahudumia kina nani? kwa hili kazana sana.
Kwa leo naishia hapa………..
at 10:31 am
Vema kaka umeonyesha nia ya kusaidia nchi yetu.Usikate tamaa mola yu pamoja nawe,kwani hata Baba wa Taifa enzi zile alisisitiza kuwa “Hakuna anayetutaka kuwapenda wenzetu kuliko tunavyo jipenda ila sisi tuliobahatika kupata elimu tunao wajibu wa kuziboresha jamii tunamotoka”
at 12:50 pm
SHIKAMOO,MH!DEWJ MM NI MWANAFUNZI NILIYEHITIMU F6 2011,MWENGE HIGH SCHOOL(SINGIDA),VP KUHUSU ILE AHAD YAKO ULIYOAHD MWENGE KWA MWANAFUNZI ATAKAE KUWA WA KWANZA?
at 11:41 am
Assalam Aleikum, nampongeza mheshimiwa mbunge. Napenda kuiomba serikali isaidie elimu ya juu kwa vijana wote maana mchango mkubwa ‘MO’ umetokana na elimu aliyoipata ya ngazi ya chuo na ndiko kipaji chake kilipojulikana. Songela baba kwa misaada yako.
at 9:37 am
Nampongeza Mh Mbunge kwa kazi anayofanya. Twamuomba afikishe pia malalamiko yetu kwa wizara husika kuhusu wanavyuo wanaoonewa na hata “kufelishwa” kwa chuki binafsiau wanapokataa kutoa rushwa ya ngono, nk.
Ili kukomesha hili twashauri karatasi za mitihani ya wanavyuo ziwe wazi ni ziweze kuangaliwa na lecturers “huru” pindi mwanafunzi anapolalamika kuonewa. Aidha lecturer ambae wanafunzi wengi wanafeli somo lake wamulikwe
at 8:16 pm
TANZANIA SPORT AND CULTURE CONSULTANT ORGANIZATION Very happy for what your doing to empower sports in our poor country your contribution will be recorded forever please dont give up to add more effort for other sports instead to concetrate with only football ,LAKE ZONE i mean LAKE VICTORIA ZONE reque3sting you and your company to empower volleyball as well they have their program for secondary school please if your able t5o assist our programme LAKE VICTORIA CLASSIC STUDENT VOLLEYBALL TOURNAMENT VISIT OUR WEBSITE
at 11:55 am
Mh. Muhammed dewji. haya ndiyo ya kujivunia ni mfano wa kuigwa na pia zirki ya mtu hapingwi walikunyima ubunge 2000, but 2005 Allah akakupa. USHAURI TENGENEZA AKHERA YAKO SAIDIA MASIKINI, WALEMAVU, WAGONJWA BASI UTAONA KILA KITU KINAENDA SAWA TU. Hongera kwa CV nzuri sana.
at 8:39 pm
ni kiongozi mzuri,ila naomba achague timu moja ya mpira awekeze.
at 8:40 pm
naomba achague timu moja ya mpira wa miguu awekeze
at 7:24 pm
Tulikua tunawasiliana kupitia tagged ndiyo ukaniambia nitumie inf@dewjiblog.com sasa ilikua inasumbua kama kweli uko interested kuhusu hiyo site tumia hiyo mail yangu hapo
at 7:32 pm
Tafadhali ukipata unijibu,
at 5:20 am
Mr Mo no any reply
at 5:46 am
may God bless u
at 7:13 am
m.Dewji kazi unazofanya zinaonekana binafi sitokei jimboni kwako lakini kazi zako kupitia blog hii zinaonyesha dhahiri wewe ni mtendaji kazi.MFANO WA KUIGWA KWA VIJANA NA WATU WA RIKA LOLOTE
at 7:15 am
MHESHIMIWA HONGERA SANA KAZI NZURI.
at 7:49 am
EEEEHHH BAB KUBWA MHESHIMIWA!!! SONGA MBELE USIJALI MAJUNGU!!!
at 12:19 pm
Wacha uongozi si lelemama baba,
Kwanza huwezi soma IST kwa mtaala wa nje na shule za Marekani ati ukawa na mtazamo wa KITANZANIA.
Kama mtu anashindwa hata kujenga choo cha timu anayodai kuipenda. Ataiweza wapi Tanzania, case study Singida ??????????????wasingida amkeni kumekucha wazalendo?????????????????????????????
at 11:31 am
una upeo achana na mambo ya siasa bora biashara kwani siasa japo ni zawadi na ni myo kwa wananchi kwanza hupoteza muda pia huondoa thamani halisi ya maisha na upeo wa maisha yako.biashara ndo mpango mzima kuna njia nyingi za kutoka mungu ameshakuandikia biashara.work hard on it.thanks
at 5:14 pm
Asasi ya TAWOTEA inakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya kwa wapiga kura wako lakini pia kwa Watanzania wote tunaopata huduma zako.
Mh endelea Mungu atakusaidia
MWL MWANAISHA KIKWETE
M/KITI TAWOTEA
at 1:33 pm
Mhe.Dewji kwa kweli mimi ni mkazi wa DSM lakini asilimia kubwa maisha yangu yako Singida,Wilaya ya Manyoni katika Kijiji cha Sanjaranda.Ninakupongeza sana kawa juhudi zako za kuujali mkoa wako na katika kipindi cha Ubunge katika mkoa wetu umekuwa na mchango mkubwa sana si kwa jimbo lako tu hata majibo ya wabunge wenzako endelea na moyo huo huo.
Nitoe sifa kubwa sana kwa mbunge wangu wa Manyoni magharibi ndugu John Paulo Lwanji juhudi zako katika kuleta maendeleo katika jimbo lako tunaziona na tunazisikia .kazana sana baba.nasi tuko nyuma yako.Nawapongeza sana nisiwaache na wabunge wote wa mkoa wa Singida.
Sisi wakazi wa DSM kutoka Singida tunawashauri muitishe mkutano au chakula cha jioni kwa kwa wakazi wa DSM watokao mkoa wa Singida kwa ajili ya maendeleo ya mkoa wetu.Tungeshukuru sana.
Eliasy R Iloghwe.
at 1:47 pm
Mhe.Dewji niomba nitumie global yako kwa ajili ya kumpongeza Mbunge we]angu wajimbo la Manyoni Magharibi Mhe.John P Lwanji nakupongeza sana kwa mikakati endelevu ya ufuatiliaji wa majukumu ya maendeleo ya jimbo letu.Kazana sana mkuu ili jimbo letu liwemo katika majimbo yanayoendelea.Ushauri wangu kwako wewe ni Mbunge wetu angalia mbele kuhusu maendeleo usiangalie kilia,kushoto,na nyuma ni mwiko kaka wewe ni mbele tu. ili wanaosema wakose ya kusema.sisi wenye jimbo,Sanjaranda,Gurungu,Itigi,Aghomndi,Idindyandole,Mgandu,Itaraka,Ibonoa,Matanga,Kirighwani,Kamenyanga,Kitopeni,Mabondeni,Muhanga,Mbungani,Muhanga nk sanahani umeme umekatika computer yangu haina moto,Lwanji nakutakia kazi njema katika kazi zako za ubunge.
Nakutakia majukumu mema sana.
Iloghwe.
at 5:20 pm
watanzania tunahitaji viongozi wazuri kama MO na wenye elimu ya kutosha ya kuweza kuwasaidia watanzania kwa hali na mali kama alivyo yeye jambo la kujivunia kuwa na mtu kama huyu.
at 6:24 am
dah mungu akujalie na akuongeze zaidi kwani niwatu wachache sana ambao wanaweza kuwa na roho kama yako,ambao awapendi kujikweza.
at 10:31 am
Mungu akujalie na azidi kukupa afya na baraka tele, watanzania yatubidi tutambue kuwa nyota njema huonekana asubuhi tumeona jinsi MO toka alivyozaliwa mpaka sasa, je kuna swali hapo? kwa nini tusibadile?? MO ana sifa zote za uongozi wa nchi ni wakati wa vijana jamani, unajua me sielewi maana ya usemi usemmwao kila siku kuwa vijana ni Taifa la Kesho kwa nini basi wasipewe vijana kama kina Mo, washirikiane na kina Nape, Zito, Mnyika, Kafulila, Mdee na vijana wengi wapiganaji wa nchi wapo wapeni waongoze na huu ujana wao wasisubiri uzeeni???? Twaamini wazee mna busara sana muwapo pembeni na si madarakani mnavurunda jamani hebu wapeni nchi vijana waongoze, pia mkubali DUNIA imebadilika tuende na wakati……..
at 6:11 pm
NAKUTAKIA MAISHA MEMA NA MAFANIKIO MBELE YA JAMII
at 9:21 am
Mh. nakupongeza sana kwa jitihada zako za kuwasaidia wananchi. Mimi niko Zanzibar katika kijiji cha Kajengwa Makunduchi. Na sisi tunaomba utupatie msaada wa visima japo viwili katika kitongoji chetu kwani tunapata shida kubwa sana ya maji katika eneo letu. Unaweza kuwasiliana nasi kwa Moh’d Simba Hassan, P.O.BOX 1937 ZANZIBAR. Simu 0777 865958 tutafurahi na kuuenzi mchango wango iwapo utafanya hivyo.
at 8:08 am
Congratulations Hon. Mo for being named as a Young Global Leader [YGL] form Tanzania by the World Economic Forum!!
Cheers.
Mutta
at 7:37 pm
WAKATI UMEFIKA KWA VIJANA KUSAIDIWA KUJENGEWA UWEZO WA KUZALISHA AJIRA NA SI KSUBIRI KUAJIRIWA.HATUWEZI KUTOKA KAMA HATUPO TAYARI KUWAWEZESHA VIJANA KUTUMIA NAFASI NA RASILIMALI ZILIZOPO KATIKA KUENDESHA MAISHA YAO
at 5:54 pm
Ni dalili nzuri kwa taifa changa kama Tanzania kuwa na watu waliofanya mambo makubwa duniani katika nyanja zote za maisha, kiuchumi, kisiasa na kijamii.
MO umeonyesha ni kiasi gani vijana tukiwezeshwa tunaweza fanya mambo makubwa zaidi ya jamii inavyofikiria.
Congratulations!
at 9:51 pm
historia nzuri mheshimiwa wetu..najiskia vizuri kusikia role models wetu kwenye ulimwengu wa biashara wanasaidia jamii!!Mungu akuzidishie kakangu
at 10:17 am
Ndiyo mhesh!litumikie taifa kwa moyo wako wote,na kwa madhumuni ya watanzania tunaoishi chini ya dollar 1 kwa siku!MUNGU awe nawe! 2ko pai
at 4:46 pm
kweli mheshimiwa unaweza ila naomba uwasidie singida wapate uwakilishi katika ligi kuu tanzania bara.mungu akuongezee mjomba
at 4:50 pm
kaka hongera kwa hatua uliofikia, ninalo moja tu la kukukumbusha tunaomba utusaidie kwenye suala la michezo kwa upande wa singida tuko nyuma sana kimichezo, kubwa zaid kaza but kiongoz
at 2:43 pm
Ni mtanzania mwenye sifa za kutosha kabisa kwa uongozi na ya ziada ni moyo wake wa kujitolea na ubinaadam!
at 4:41 pm
Kwako kaka MO,nimekuwa nikifuatilia kwa makini sana juhudi zako za kuibadilisha Singida kwa muda mrefu sana hakika umefanya mengi yanayo hitaji pongezi.Binafsi natamani sana kuwasaidia ndugu zangu wa Singida namwomba Mungu anijalie nafasi hiyo ya kutoa mchango wangu pia.Kifupi nasema tupo nyuma yako tuijenge Singida naTaifa kwa ujumla wake
at 7:29 am
Uonapo wanaokupongeza ni wengi na wanaokuponda ni wachache. Ujue unakubalika katika jamii, endelea na moyo huohuo uliojaaliwa na Mwenyezi Mungu. Maneno ya kukuponda nisawa na maji ya moto ambayo haya wezi kuunguza nyumba uyapuuze.
at 1:12 pm
Hongera bro… keep it up..!
at 1:58 pm
KAZA BUTI!! TANZANIA YA LEO TUNAHITAJI KICHWA KAMA MOH; EEH! BWANA!EEE! USIKATE TAMAA GODBLESS U A LOT!
at 3:44 pm
PLEASE COME BACK TO OUR TEAM(SIMBA) AS SPONSOR WE REAL NEED YOUR SUPPORT. YOUR SUPPORT WILL HELP OUR TEAM TO HAVE OUR OWN GROUND